lyrics
Bwana ning’ome na Mwokozi wangu, nimwogope nani?
Alishanijua tokea utotoni, bado yupo nami.
Nilipopita kwenye giza, mkono wake ukanishikili,
Nilipoanguka chini, rehema zake zikaninyanyua tena.
Wengi waliondoka, yeye hakuwahi kuniacha,
Milango ilipofungwa, yeye akanifungulia njia.
Nililia kimya, lakini yeye alisikia,
Nilipokosa nguvu, akaniambia “simama.”
Chorus
Nani kama wewe, Bwana wangu?
Nani wa kunishika nikitetemeka?
Tokea utoto mpaka leo,
Mikono yako bado iko nami.
Sina cha kujivunia zaidi ya neema,
Kila pumzi ninayovuta ni zawadi yako, Baba.
Wakiniona leo wakisema nimeweza,
Mimi najua ni wewe uliyenifikisha hapa.
Nitaimba mpaka sauti yangu ichoke,
Nitasifu mpaka machozi yashuke.
Maana maisha yangu ni ushuhuda,
Kwamba Mungu wangu hajawahi kuniacha.